Makamu wa Rais asisitiza umuhimu wa kutunza maji
Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, amesisitiza umuhimu wa kubuni mifumo na mbinu za kutunza vyanzo vya maji na ardhi oevu, akieleza kuwa matumizi ya maji kwa binadamu, mifugo, na wanyamapori yanapaswa kuzingatiwa kwa usawa.