Askofu Mokiwa aonya tatizo la ukosefu wa ajira
Aliyekuwa mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini Tanzania, Askofu Valentino Mokiwa, ameonya juu ya kuongezeka kwa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana, ambapo amefananisha tatizo hilo kuwa ni sawa na bomu linalosubiri kufyatuka wakati wowote.