Mgombea Ubunge CCM aahidi utoaji mikopo kwa vijana

Alhamisi , 15th Oct , 2020

Mgombea ubunge wa Jimbo la Ulanga Salim Hasham Alaudin amesema ili kumkomboa kijana katika ombwe la umaskini ni kumuwezesha kupata nyenzo Bora ambazo atazifanyia kazi hasa katika sekta ya viwanda na kilimo.

Kushoto ni mgombea ubunge wa Jimbo la Ulanga Salim Hasham Alaudin

Aliyesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya iragua wakati wa kampeni za wagombea wa chama Cha mapinduzi wilayani Ulanga.

Alisema kwa sasa nchi inatekeleza Sera ya viwanda na ili kufanikiwa lazima kutengeneza mazingira Bora ya upatikanaji wa malighafi ambazo kwa mkoa wa morogoro nyingi hutoka katika kilimo.

Aliongeza kusema kuwa mbali na matrekta pia  utoaji wa mikopo ya vikundi kwa ajili ya kilimo kwa vikundi utaendelea ambapo anasema tayari alikwishaanza kutoa mikopo hiyo.

"Najua vijana wenzangu mnajua nilishaanza na nyie Siku nyingi tu kutoa hii mikopo kwa ajili ya vikundi nitaendelea kuwasapoti mpaka kieleweke nataka baada ya miaka mitano ijayo mapori haya yote yageuke mashamba"alisema Salim Hasham Alaudin

Mbali na kilimo kwa vijana mgombea huyo wa ubunge alisema tayari ilani ya uchaguzi ya chama Cha mapinduzi imesisitiza kufanya kazi na kuunga mkono jitihada za mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ataendelea kusisitiza ufanyaji wa kazi hasa kwa vijana ambao ndiyo nguzo kubwa ya uchumi.

"Niwaambie tu mnaona maandalizi ya kuanza kazi kwa kampuni za uchimbaji madini kila kitu kipo sawa Ila tunasubiri leseni tu kuanza kazi kampuni hizo amini ajira zitakuwa za kumwaga hapa zaidi ya 300 sasa vijana wetu wataajiriwa kwa kazi za muda mrefu haya yote ni matunda ya uongozi thabiti wa mgombea wetu Dk.John Pombe Magufuli"alisema  Salim Hasham Alaudin