Paresso ashindwa ubunge jimbo la Karatu

Ijumaa , 30th Oct , 2020

Aliyekuwa mbunge wa viti maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Cecilia Daniel Paresso, ameshindwa kuchukua ubunge aliokuwa akiupigani wa jimbo la Karatu Mkoani Arusha baada ya Daniel Awaki wa Chama cha Mapinduzi,(CCM), kushinda jimbo hilo.

Aliyekuwa mbunge wa viti maalum na mgombea ubunge jimbo la Karatu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Cecilia Daniel Paresso

Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Karatu amemtangaza Daniel Awaki, wa CCM kuwa mshindi wa jimbo hilo ambaye amepata kura 49,042 akifuatiwa na Cecilia Daniel Paresso, wa CHADEMA, aliyepata kura 31,150 

Aidha idadi ya wagombea ubunge katika jimbo la karatu walikuwa sita kutoka vyama vya CCM, NLD, CHAUMMA, NCCR MAGEUZI, ACT WAZALENDO na CHADEMA.