Je, historia imewabeba mawaziri wa JPM?

Ijumaa , 30th Oct , 2020

Katika awamu yake ya kwanza Rais John Magufuli, aliunda Baraza lake la kwanza la Mawaziri tarehe 10 Desemba 2015 ambalo alilitangaza kwa awamu mbili huku likiwa na mawaziri 19 katika wizara 18 ambapo katika orodha hiyo hakuwa amezijaza nafasi nne za uwaziri ambazo alizijaza wiki mbili,

Pichani ni Wabunge wateule, kushoto ni Mh. Jenista Mhagama (Peramiho), Mh. Ummy Mwalimu (Tanga Mjini), kulia ni Mh Dkt Philip Mpango (Buhigwe).

baadaye tarehe 23 Desemba.

Katika awamu yake ya kwanza ya kipindi chote cha miaka mitano Rais Magufuli alifanya mageuzi kadhaa yakiwemo mageuzi makubwa kwa madogo katika nafasi za uwaziri ikiwemo kuwaondosha kabisa mawaziri kwenye baraza au kuwahamisha na kuwabadilisha wizara huku wengine wakiwa hawajaguswa kwa kipinde chote cha miaka mitano zaidi wakisifiwa kwa utendaji wao.

Mawaziri hao sita ambao waliweza kuepukana na wimbi la tumbua tumbua pia walijitokeza katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi za ubunge katika maeneo yao, kando na Dkt. Hussein Mwinyi aliyejitosa kuwania Urais huko Visiwani Zanzibar na kuibuka na ushindi wa kura 380,402.

                                          Rais Mteule wa Serikali ya Mpinduzi Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi

Mawaziri hao ni pamoja na Dkt. Philip Mpango (Wizara ya Fedha na Mipango), Prof Joyce Ndalichako, (Elimu), Wiliam Lukuvi (Ardhi na Maendeleo ya Makazi), Jenista Mhagama (Sera, Bunge,Vijana) na Ummy Mwalimu (Afya).

Pichani ni Wabunge Wateule, Kushoto ni Mh.William Lukuvi (Isimani), kulia ni Mh Prof Joyce Ndalichako (Kasulu Mjini)

Aidha wabunge hawa ambao utendaji wao katika wizara zao ulitajwa kuwa wa mfano pia kumpendeza Rais, tayari wametangazwa kushinda katika majimbo yao ambapo Mpango amepata kura (Buhigwe 43,481), Ndalichako (Kasulu Mjini 49,390), Lukuvi (24,934), Mhagama (Peramiho, 27,479), Ummy (Tanga Mjini114,445).