Magufuli Rais mteule wa Tanzania 2020 - 2025

Ijumaa , 30th Oct , 2020

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, leo Oktoba 30, 2020, amemtangaza Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wa CCM, kuwa mshindi wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kupata kura milioni 12,516,252.

Rais mteule wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

Magufuli ameshinda uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 28, 2020 ukijumuisha madiwani na wabunge, ambapo jumla ya majimbo 264 yameshiriki uchaguzi huo.

Mwenyekiti huyo wa Chama Cha Mapinduzi, anaingia katika awamu yake ya pili ya uongozi, baada ya awamu ya kwanza kuanza mwaka 2015 na kumalizika 2020 na sasa ataendelea kwa kipindi cha 2020 hadi 2025.

Jumla ya vyama 15 vilishiriki uchaguzi ngazi ya urais na mpinzani aliyemfuatia Magufuli kwa ni Tundu Lissu wa CHADEMA ambaye amepata kura 1,933,271.

Orodha kamili ya wagombea urais na kura walizopata
1.    Philipo Fumbo (DP) - 8283
2.    Leopold Mahona (NRA) - 80787
3.    John Shibuda (Ada Tadea) - 33,086
4.    Hashim Rungwe (CHAUMMA)-32,878
5.    Queen Sandiga (ADC) - 7627
6.    Seif Maalim Seif (AAFP) - 4635
7.    Twalib Kadege (UPDP) - 6194
8.    Muttamwenga  Mgaywa (SAU) - 14922
9.    Cecilia Mmanga (Makini) - 14556
10.    Khalifan Mazurui (UMD) -3721
11.    Yeremia Maganja (NCCR) - 19969
12.    Profesa Ibrahimu Lipumba (CUF) - 72885
13.    Bernard Membe (ACT) - 81,129
14.    Tundu Lissu (Chadema) - 1,933,271
15.    Dr. John Pombe Magufuli (CCM) - 12,516,252
 

Tazama Video hapo chini akitangazwa