Zitto akamatwa, ACT Wazalendo yaeleza undani

Jumanne , 3rd Nov , 2020

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni leo Novemba 3, 2020, na anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay.

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe

ACT Wazalendo wameeleza kuwa Zitto alifika kituoni hapo kuwaona viongozi wa vyama vya upinzani ambao wanashikiliwa na jeshi hilo.

Viongozi wengine ambao Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa, ameeleza wanashikiliwa tangu Novemba 2, 2020 ni Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe.

Wengine ni aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema na Meya wa zamani wa Ubungo Boniface Jacob.