Region: 
Dar es salaam
District: 
Ilala District
Donation: 
Taulo za kike kwa wanafunzi 54 mwaka mzima

Katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, kampeni ya Namthamini ilitembelea Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko na kufanikiwa kutoa mchango wa taulo za kike ambazo zitawawezesha wanafunzi 54 kusoma bila kikwazo kwa mwaka mzima.