Alhamisi , 6th Oct , 2022

Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam limekemea vikali ubadhilifu wa vifaa vya Ujenzi kwenye miradi mbalimbali ya Jiji Hilo na kuziagiza kamati za ujenzi kufanya Udhibiti kikamilifu ili miradi hiyo ikamilike Kwa wakati na ubora uunaotakiwa

Mkuu wa wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija.

Mkuu wa wilaya ya Ilala Ludigija katika ziara ya kukagua miradi  amesema kumekuwa na ujanja ujanja wa baadhi ya wakandarasi kufanya udanganyifu wakati wa kuagiza vifaa vya Ujenzi ikiwemo mchanga na kokoto  hivyo kukwamisha Kasi ya Ujenzi wa miradi Kwa wakati na  kuisababiashia serikali harasa ya kujenga mara mbilimbili

"Sasa tumeamua kupitia kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ilala tutahakikisha tunafuatilia Kwa karibu miradi yote inayotekelezwa  ili ijengwe Kwa ubora kama mikataba inavyoelekeza" amese Ng'wilabuzu Ludigija-Mkuu wa wilaya ya Ilala

Ziara ya Kamati yavukinzi na usalama imefanyika Kwa siku mbili ambaoo imekagua Ujenzi wa vituo vya afya ambayo vinajengwa Kwa fedha za tozo,Ujenzi na upanuzi wa soko la kigogo fresh ambalo kinajengwa wa fedha za uviko sambamba na Ujenzi wa shule ya sekondari Liwiti ambayo inajemgwa Kwa mtindo wa ghorofa na mradi wake utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.4