Mwaka 2017 East Africa Television LTD ilianzisha kampeni ya kuchangisha taulo za kike kwa wanafunzi wenye uhitaji shuleni.
Kampeni hii ilikuja baada ya tafiti kuonesha kuwa wasichana wengi hupata changamoto katika siku zao za hedhi kwa kushindwa kununua taulo za kike hivyo kupelekea kukosa masomo shuleni kwa takribani siku 3 mpaka 7 kwa mwezi za masomo.
2022 ni mwaka wa sita (6) tangu kuanzishwa kwa mradi huu, huku lengo kuu likiwa kumuweka msichana shule bila kukosa sababu ameshindwa kununua taulo salama za kujihifadhi.
Mwaka huu 2022, kampeni hii ina lengo ya kufikia watoto wa kike 5000 katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania.
Lengo la Kampeni
Lengo letu kuu ni kumsaidia msichana huyu kwa kumpatia taulo salama na kuhakikisha hakosi tena masomo yake na anafikia ndoto zake.
'Unapomuinua mtoto mmoja wa kike, umeinua jamii nzima'
#Namthamini
#NasimamaNaye