Ijumaa , 27th Aug , 2021

Kuelekea Tuzo za Tehama Tanzania, Mkurugenzi wa Tume ya Tehama Tanzania, Samson Mwela, amesema lengo la tuzo hizo ni kuibua na kukuza vipaji vya wabunifu wa tehama nchini ili kutengeneza taifa la kidijitali.

Mkurugenzi wa Tume ya Tehama Tanzania, Samson Mwela (aliyesimama) akitoa mafunzo kwa Wanahabari na Watangazaji wa East Africa Television na East Africa Radio.

Mwela ameyasema hayo leo Agosti 27, 2021 wakati akitoa mafunzo kwa Wanahabari na Watangazaji wa East Africa Television na East Africa Radio juu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na tume hiyo ikiwemo Tuzo za Tehama Tanzania (ICT Awards 2021).

''Kwenye hizi tuzo sio tu tunaangalia wasomi au taasisi ambazo tayari zimeshafanikiwa, tutawafikia wabunifu wengi chipukizi ndio maana tuna vipengele takribani 18 tu kuwatambua wote pamoja na kuzikuza kazi zao ambao kwa namna moja zimeleta suluhu ya changamoto nyingi kwenye jamii'', amesema.

Mkurugenzi wa Tume ya Tehama Tanzania, Samson Mwela (aliyesimama) akitoa mafunzo kwa Wanahabari na Watangazaji wa East Africa Television na East Africa Radio.

Aidha ameeleza kuwa kwasasa zoezi linaloendelea ni watanzania wenyewe kupendekeza majina ya watu au kampuni za watoaji wa huduma bora wa Tehama nchini, kupitia tovuti ya tume https://www.ictc.go.tz/ na litamalizika Septemba 10, na kuanzia Septemba 11 hadi 18 waliopendekezwa watajaza fomu maalum wakieleza nini wamefanya kisha utaratibu wa kuwapigia kura utatolewa.

Picha ya pamoja ya Mkurugenzi wa Tume ya Tehama Tanzania, Samson Mwela na Wanahabari na Watangazaji wa East Africa Television na East Africa Radio.

Kupitia kituo kilichozinduliwa cha Soft Centre watanzania wabunifu wa tehama wanaendelea kusajiliwa ili watambulike na kazi zao zitambulike ikiwemo kupewa nguvu ya kufikisha mbali zaidi kazi zao, hivyo umetolewa wito watu wachangamkie fursa hiyo.