Alhamisi , 24th Nov , 2022

Serikali imetenga shilingi bilioni 400 kwa ajili ya kuanzisha kilimo cha umwagiliaji ili kufikia lengo la kumwagilia hekta milioni 10 ifikapo mwaka 2030.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde katika jukwaa la kilimo kwa ukanda wa Afrika mashariki na kusini mwa Afrika ambapo Tanzania ni mwenyeji wa mkutano huo ulioanza leo jijini Dar es salaam huku serikali ikipanga kununua ndege ya kumwagilia dawa mashambani

Mavunde amesema takribani mabonde 22 yote utekelezaji umeanza nchi nzima ikiwa ni jitihada za kupambana na ukame pamoja na mabadiliko ya Tabia nchi

Kwa upande wake Mwenyekiti wa SACAU ambao hujumuisha ukanda wa nchi za SADEC Dkt Yusuph Sinare amesema mkutano huo umewakutanisha wafadhili kwenye sekta ya kilimo IFAD ili kurekebisha sekta ya Kilimo hususani kwa vijana ambao ndio walengwa wa serikali kwa masilahi mapana yao na Taifa

Uanzishwaji huo wa mabwawa unatarajiwa kutunza lita bilioni 111