Jumatatu , 9th Aug , 2021

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdallah amesema serikali haitomvumilia mfanyabishara yoyote atakayekwenda kinyume na bei elekezi zinazotolewa na Serikali.

Picha: Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman (wa pili kushoto)

Kauli hiyo inakuja kufuatia viongozi na wanachama wa CCM kuiomba serikali kulipatia ufumbuzi tatizo la kupanda bei bidhaa lilitolewa katika kikao maalum kilichofanyika katika ofisi za CCM Amani Mkoa.

"Tumegundua kuna ujanja unafanywa na wafanyabiashara, na hatutaki kuona bei hizo zinapanda kiholela kinyume na utaratibu viongozi wenzangu nakuombeni msione serikali imekaa kimya, serikali tupo makini kwa hilo na tunalisimamia hilo ipasavyo na hatutomuonea haya au vibaya mtu yeyote ambaye atakiuka utaratibu na maelekezo ya serikali," amesema Mhe. Hemed.

Pia Mhe. Hemed alisema kuwa Serikali imeshatoa maelekezo kwa Wizara husika kwa ajili ya kupanga namna bora ya bei za bidhaa ili zisiwaumize wananchi kwa ujumla.