Jumatano , 24th Dec , 2014

Milio ya risasi zilizokuwa zikifyatuliwa na askari wa jeshi la polisi jana ilirindima katika soko kuu la Kariakoo, jijini Dar es Salaam na kuzua taharuki kwa wafanyabiashara, wateja na wapita njia katika eneo hilo.

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki.

Hali hiyo imekuja baada ya Wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Wamachinga kufunga mtaa na kupambana na askari wa halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa kupinga kuondolewa na askari hao kandokando ya soko hilo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Ilala, Mary Nzuki, amesema kutokana na hali hiyo jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala linawashikilia watu 24 kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo.

Kamanda Nziki alisema chanzo cha vurugu hizo kuwa ni wamachinga hao ambao walikuwa wakifanya biashara barabarani kuzuiwa na askari wa jiji, lakini waligoma kuondoka na kuanza kufanya vurugu.