Jumanne , 29th Apr , 2014

Watu 19 wa kijiji cha Utaho wilayani Ikungi wamepoteza maisha wakiwemo askari wanne wa jeshi la polisi, baada ya kugongwa na basi la summry

SACP Godfrey Kamwela, Kamada wa polisi mkoa wa Singida

Watu 19 wa kijiji cha Utaho wilayani Ikungi wamepoteza maisha wakiwemo askari wanne wa jeshi la polisi, baada ya kugongwa na basi la summry wakati wakiwa wanatoa msaada wa kumpakia marehemu kwenye gari la polisi aliye gongwa na gari kubwa ambalo halikufahamika mara moja.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa jeshi la polisi mkoani singida SACP Geofrey Kamwela, amesema  ajali hiyo ambayo imetokea katika kijiji cha Utaho Wilayani Ikungi, ilianza kwa lori kumgonga mtembea kwa miguu na kufariki papo hapo.

SACP  Kamwela amesema wakati askari na wananchi wakifanya utaratibu wa kuitoa maiti hiyo na kuiweka kwenye gari la polisi, ndipo lika fika basi  la Sumry lenye usajili wa namba T 799 BET na  ghafla likatoka nje ya barabara na kuwagonga watu waliokuwa wamefika eneo hilo na kuwakanyaga na kusababisha vifo vya watu hao. 

Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa singida  Dkt Musa Kimala ,amesema awali wamepokea maiti 14 na nyingine tano zilikuwa zipo katika hospita ya misioni ya Malkia wa ulimwengu Puma  na majeruhi wawili ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa singida  wamepatiwa matibabu na wengine sita wanapatiwa katika hospitali ya mision ya Malkia wa ulimwengu puma.

Wakielezea baadhi ya watu walio shuhudia ajali hiyo akiwemo mchungaji Adulile Mbwile ambaye alikuwa abiria wa basi la Sumry  amesema waliona gari la polisi likiwa barabarani na walipotaka kulipita upande wa kulia, wakaona kuna gari lingine linakuja ndipo dereva alipoamua kulipitisha basi upande wa kushoto na kuwapitia watu ambao walikuwa nje ya barabara 

Ajali hiyo ambayo ni ya kutisha na kusababisha vifo vya watu wengi kwa mara moja EATV imeshuhudia kuona miili katika eneo la ajali ikiwa vichwa vimepasuka, miili imevunjikavunjika na baadhi ya maiti  zimetengana vichwa na miiili.

Ajali kama hiyo mbaya  kwa mwaka huu ni ya pili kutokea, ambapo mwanzoni mwa mwaka huu basi dogo aina ya Noah iligongana na lori na kusababisha vifoo vya watu 13 wilayani Ikungi