Jumanne , 30th Nov , 2021

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Uganda Fred Enanga, amesema kwamba jeshi hilo linamshikilia mwanaume mmoja aitwaye Paul Mubiru, ambaye video zake zilisambaa mitandaoni akiuza Senene ndani ya Ndege ya Shirika la Ndege la Uganda iliyokuwa ikielekea Dubai.

Senene

Aidha, Jeshi hilo pia linamshikilia Hajib Kiggundu, ambaye yeye alihusika katika kurekodi video hiyo.

Kupitia mitandao ya kijamii hivi karibuni zilisambaa video zikionesha Mubiru akiuza Senene, ambapo abiria wengi walionekana kufurahia huduma hiyo kutoka kwake.