
Msemaji wa polisi nchini Uganda Fred Enanga akizungumza na wanahabari Jijini Kampala nchini Uganda
Msemaji wa polisi nchini Uganda Fred Enanga amesema mwanamke huyo mkazi wa Tarafa ya Makindye jijini Kampala anatuhumiwa kusababisha kifo cha Benson Baluku ambaye alikuwa akiishi naye kama mume
Kwa mujibu wa polisi, marehemu alirejea nyumbani Machi 26 akiwa amelewa na kuanza kupigana na mkewe ambaye kila mara alimtuhumu kuwa na mahusiano ya nje ya ndoa.
Polisi wamesema mume alimshika mkewe shingoni na kuanza kumnyonga hali iliyomfanya mke atoe kisu na kumkata sehemu za siri