Awauwa baba, mama na ndugu zake wawili

Jumanne , 12th Jan , 2021

Lawrence Waruinge na mpenzi wake wamefikishwa mbele ya makahakama Kaunti ya Kiambu, Kenya, kutokana na mauaji ya watu wa tano wote wa familia ya Lawrence, akiwemo baba yake mzazi, mama yake mzazi, ndugu zake wawili pamoja na mfanyakazi wa ndani.

Kijana Lawrence Waruinge (kushoto) na mpenzi wake (kulia)

Mauaji hayo anatuhumiwa kutekeleza Lawrence wiki iliyopita na amekiri kuyatekeleza mauaji hayo. Baada ya kukiri, sasa siku ya Alhamisi Januari 14, 2021, atafanyiwa uchunguzi wa akili kabla ya kesi yake kuanza.
Baada ya kukiri kutekeleza unyama huo Lawrence aliwapeleka maafisa wa upelelezi hadi pale alipo ficha vifaa alivyotumia kwenye mauaji hayo, akisema kuwa aliamua kuchukua hatua hiyo, kutokana na kile alichokitaja kama kubaguliwa na familia yake.

Kijana huyu mwenye umri wa miaka 22, atafikishwa tena mahakamani tarehe 25 mwezi huu baada ya uchunguzi kukamilika, pamoja na mpenzi wake, anayesemekana kukodisha chumba walichotorokea kabla na baada ya maujaji, wote wakishtakiwa kwa kosa la mauaji.

Zaidi tazama video hapo chini