Ijumaa , 27th Jun , 2014

Siku mbili kabla ya kuanza kwa mfugo wa Ramadhani,bei za bidhaa mbali mbali zinazotumika zaidi kwa mfungo wa huo hazijapanda tofauti na miaka ya nyuma.

Vyakula kama vinavyoonekana sokoni.

East Afriika Radio imetembelea bafhi ya masoko likiwemo la Karikakoo,Tandale na Buguruni na kukuta bidhaa hizo zikuzwa kwa bei ya kawaida.

Kilo moja ya viazi mviringo mpaka jana ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi 1,00 kwa kilo,Mchele shilingi 2000 kwa Kilo,Maharage shilingi 2,500 kwa kilo.

Wakati huohuo, madereva wa daladala zinazotumia barabara ya Shekilango kuelekea kituo cha makumbusho wakitokea Posta na Kariakoo Jijini Dar es Salaam, wameelezea kuendelea kuzorota kwa biashara tangu kuamishwa kwa kituo cha mabasi cha Mwenge.

Wakiongea leo jijini Dar es Salaam katika kituo cha mabasi cha chuo cha ustawi wa jamii, madereva hao Bw. Abeid Ngwele na Hamidu Swalehe amesema gharama za uendeshaji zimekuwa kubwa sambamba na kupungua kwa abiria wanaowabeba.

Katika mahojiano na East Africa Radio, madereva hao wameiomba mamlaka ya usafiri wa nchikavu na majini (Sumatra) kuja na utaratibu ambao utawarahisishia kufanya biashara yao ya usafirishaji pasipo kusababisha kupungua kwa mapato na kufanya biashara kwa hasara.