Jumanne , 17th Mei , 2016

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye amesafirishwa kutoka Moroto ambako amekuwa akizuiwa tangu Jumatano iliyopita hadi jela yenye ulinzi mkali ya Luzira katika mji mkuu wa Uganda jana

Wakili wa Kiiza Basigye, Ladislaus Rwakafuuzi akiongea na waandishi wa Habari

Msemaji wa Idara ya Mahakama wa Uganda Solomon Muyita amesema Besigye atafikishwa mahakamani tarehe 25 mwezi huu.

Kiongozi huyo anashitakiwa kwa uhaini baada ya kujiapisha wiki iliyopita kuwa Rais wa Uganda.

Iwapo atapatikana na hatia, hukumu ya uhaini ni adhabu ya kifo. Awali jana wakili wa Besigye alisema anawasiwasi na usalama wa mteja wake.

Ladislaus Rwakafuuzi amesema kuna hofu kuwa huenda kuna njama ya kumpa sumu Besigye.