Alhamisi , 24th Nov , 2022

Wanafunzi watatu wa shule ya msingi Buhangija na kituo cha elimu maalumu Buhangija Manispaa ya Shinyanga wamepoteza maisha, baada ya bweni la wasichana walilokuwa wamelala kuungua moto usiku wa kuamkia leo  huku wengine wakinusurika baada ya kuokolewa

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amethibitisha kutokea tukio hilo ambapo amesema moto huo umeanza kuwaka majira ya saa tano  usiku wakati wanafunzi hao wakiwa wamelala ndani ya bweni hilo lililokuwa na watoto 32

Kufuatia tukio hilo Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linafanya uchunguzi wa chanzo cha moto huo kwa kushirikiana na mamlaka nyingine ili kubaini kilisababishwa na nini