Jumanne , 21st Sep , 2021

Jeshi la Polisi nchini Kenya linaendelea na uchunguzi wa mauaji ya watoto wawili wanaodaiwa kuuawa na baba yao ambaye ni Daktari Mjini Nakuru, huku mshukiwa akiendelea kupokea matibabu baada ya kuzirai kwenye eneo la tukio.

Daktari

Tukio hilo linadaiwa kutokea siku ya Jumapili ambapo hadi sasa bado familia ya daktari huyo James Gakara haijaamini matukio ya siku hiyo, na ni nini kilichompelekea daktari huyo kuwauwa watoto wake.

Polisi wameeleza kuwa walifika eneo la tukio na kukuta watoto hao wa miaka mitatu na mitano wakiwa wamefariki, huku Daktari Gakara ambaye ni Baba wa watoto hao ambaye pia ni mshukiwa wa mauaji hayo akiwa amepoteza fahamu.