Jumatatu , 16th Mei , 2022

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amesema hadi kufikia Desemba 2022 Tanzania inakadiriwa kuwa na Watanzania milioni 1.7 ambao wanaishi na virusi vya Ukimwi na kati yao milioni 1.5 wameweza kutambua hali zao.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

Kauli hiyo ameitoa leo Mei 16, 2022, bungeni jijini Dodoma, wakati wa uwasilishaji wa makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2022 hadi 2023 na kusema hadi sasa asilimia 95.8 ya wanannchi waliokuwa wanatumia dawa za ARV walikuwa wamefubaza wingi wa virusi vya Ukimwi ambayo ni sawa na chini ya nakala 1000.

"Hadi Desemba 2022, nchi yetu inakadiriwa kwamba kuwa na watanzania milioni 1.7 ambao wanaishi na virusi vya Ukimwi," amesema Waziri Ummy

Aidha Waziri Ummy, amemshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kwa kuwa balozi wa kuhamasisha wanaume kupima virusi vya Ukimwi.