Alhamisi , 15th Oct , 2015

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jayaka kikwete leo atawaongoza wakazi wa Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla katika Mazishi ya Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Marehemu Dkt. Abdalah kigoda.

Dkt.Mohammed Gharib Bilal akiongoza waombolezaji kuaga mwili wa Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda jijini DSM

Akiongea wakati wa kuaga mwili mapema leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mussa Uledi amesema taifa limepoteza kiongozi msomi mwenye maono makubwa ya kuleta mapinduzi katika sekta ya viwanda na biashara hapa nchini.

kwa upande wa kaimu katibu mkuu wa CHADEMA Salum Mwalimu amesema Marehemu Dkt. Kigoda alikuwa ni kiongozi asiyependa makuu na mwenye kushirikiana na kila mtu bila ubaguzi wowote na atakumbukwa sana kwa uchapakazi wake.

Mazishi hayo yatafanyika nyumbani kwake wilaya ya Handeni leo saa 9 Alasiri na yatahudhuriwa na viongozi wa serikali na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa.

Marehemu Dkt Abdallah Kigoma enzi za uhai wake