Jumatano , 6th Jul , 2022

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, amemsimamisha kazi mkuu wa idara ya ujenzi na msimamizi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Ukerewe mkoani mwanza Mhandisi Paul Koroso kwa kushindwa kutoa mchanganuo wa matumizi ya fedha za ujenzi huo ambazo ni shilingi bilioni 2.7.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel

Dkt. Mollel ametoa kauli hiyo wilayani Ukerewe baada ya Mhandisi Koroso kutoa majibu na lugha ya kijeuri kuwa hajali lolote hata kama akitumbuliwa

"Ni kwamba tunatoka kwenye hii ofisi wewe siyo mkuu wa idara ya ujenzi kwenye hii wizara tuko pamoja? tumemaliza hiyo, kwahiyo Katibu Mkuu namtumia ujumbe mkuu wa idara atakayekuja kusimamia na kushirikiana na hii timu atakuwa mwingine na atakayesimamia hii idara atakuja mwingine," amesema Dkt. Mollel

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Kanali Denis Mwila, amesema mambo ya sintofahamu katika ujenzi huo yametokana na mkuu huyo wa idara kutotambua ofisi yake na kujifanyia kazi bila ushirikiano.