Alhamisi , 15th Oct , 2015

Mgombea Mwenza wa urais wa Tanzania kupita Chadema anayeungwa mkono na UKAWA, Mh. Juma Duni Haji amewataka wagombea wa ubunge katika majimbo tofauti kuheshimu maamuzi ya viongozi wa UKAWA ya kuachiana majimbo ili kuepuka kugawana kura.

Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania kupita Chadema anaeungwa mkono na UKAWA,Mh. Juma Duni Haji

Akiongea katika mikutano ya hadhara katika majimbo ya Buyungu na Kasulu Mjini, mkoani Kigoma baada ya kushindwa kuwanadi wagombea wa majimbo hayo kupitia chama cha NCCR-Mageuzi baada ya wananchi kudai hawakubaliki na wanaokubalika ni wagombea wa CHADEMA.

Mh. Juma Duni Haji amesema katika kugawana majimbo hayo CHADEMA wana majimbo mengi zaidi hivyo katika maeneo mengine wagombea hawanabudi kufuata maagizo ya viongozi wao ili kuepuka kugawana kura na kukipa ushindi chama cha mapinduzi.

Mzee duni ameongeza kuwa CHADEMA peke yake wanamajimbo yasiyopungua 148 hivyo amewataka wagombea wengine waweze kuwasaidia wagombea walioteuliwa na umoja huo katika kufanya kampeni.

Kwa upande wake Aliyekuwa mbunge wa Mkanyageni kupitia CUF, Habib Mnyaa amewataka wanachama wasikubali kuchanganyana katika majimbo na kusema zote hizo ni hujuma za chama cha mapinduzi kutaka kuwavuruga.