Jumamosi , 25th Sep , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, leo amerejea nchini akitokea Jijini New York Marekani, alikohudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusema kwamba Tanzania imepata nafasi ya kushiriki mkutano huo na Dunia inawasalimia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Akizungumza hii leo Septemba 25, 2021, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, amesema kuwa amepata nafasi ya kuzungumza na viongozi mbalimbali na kuwasihi Watanzania kushikamana katika kulijenga Taifa.

Tazama video hapa chini