Alhamisi , 24th Nov , 2022

Shirika la Afya duniani WHO limesema hadi kufikia Novemba 23 mwaka huu idadi ya wagonjwa wa UVIKO 19 duniani ni milioni 635 na vifo milion 6.6 huku kwa Afrika wagonjwa wamefikia zaidi ya milioni 9.3 

Mtaalamu wa chanjo kutoka shirika la afya duniani WHO Dk. Caroline Akim amesema licha ya maambukizi ya UVIKO 19 kuendelea kupungua siku hadi siku lakini ameendelea kuwaasa wananchi hususani vijana ambao wanaimani kuwa hawawezi kupata maambukizi kwa haraka kuchukua tahadhari ili kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo.

Naye mganga mkuu wa mkoa wa Pwani Dk. Gunini Kamba amesema hivi sasa wameanza kuhamasisha wananchi ikiwemo kuwafuata wananchi katika makazi yao kwaajili ya kuwapatia chanjo ili kuepukana na uwezekano wa kupata virusi vya UVIKO 19