Alhamisi , 21st Apr , 2016

Watanzania wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi wametakiwa kufuata taratibu zilizowekwa na serikali kupitia wakala wake ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza hususani wakati wanapopata matatizo wakiwa huko.

Waziri wa nchi Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Muhagama,

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa leo Bunge Mjini Dodoma na Waziri wa nchi Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Muhagama, wakati akijibu swali la Mbunge wa Chambani Yusuph Salum Hussein, kuhusu utaratibu gani utatumika kuwatafutia kazi nje ya nchi Watanzania.

Mhe. Mhagama amesema serikali imeweka wakala wa serikali wa huduma za Ajira Tanzania(TAESA), na kurasimisha wakala binafsi wa huduma za ajira ambao wana jukumu la kuwaunganisha watafuta kazi na waajiri wa ndani na nje ya nchi.

Waziri Mhagama mpaka sasa Takwimu za wafanyakazi wanaofanyakazi nje ya nchi ambao wamefuata utaratibu wa serikali ni kupita wakala wa wa Taesa ni wafanykazi 4992 ambao wako katika mataifa mbalimbali wakifanya kazi.