Ijumaa , 5th Aug , 2022

Gari aina ya Harrier lenye namba T 210 DRC, limepata ajali baada ya kumvamia bodaboda aliyekuwa amepaki pembeni katika makutano ya barabara ya ITV jijini Dar es Salaam, na kusababisha uharibifu wa vyombo hivyo vya moto.

Gari lililogonga bodaboda

Ajali hiyo imetokea hii leo Agosti 5, 2022, ambapo kwa mujibu wa mashuhuda gari hilo liligongwa kwa nyuma na kukosa mwelekeo ambapo ilipelekea kuvamia pikipiki iliyokuwa imepaki pembeni na dereva wake.

Katika ajali hiyo hakuna kifo wala majeruhi, lakini gari hilo limeharibika kwani tairi zake mbili za nyuma zimepasuka na pikipiki kuharibika.