
Mbunge huyo ametoa vifaahivyo vya michezo katika Shule 13 za Sekondari na Shule za Msingi karibu 50 za Jimbo la Manonga.
"Kwa kuanzia Tumezipatia Vifaa vya Michezo kama Mipira ya Footballs, Netballs, Basketballs, Handballs na Volleyballs,"Jumla ya Mipira 180 tumegawa nikiwa kama Mbunge wa Jimbo la Manonga ikiwa na lengo la kukuza na kuboresha sekta ya Michezo Jimboni". Amesema Mh. Seif Khamis Gulamali
Mh Gulamali amesema hii itapelekea kukuza Viwango vya wanamichezo katika jimbo la Manonga na wilaya ya Igunga kwa ujumla ndio maana ametoa vifaa hivyo