Ijue sababu ya wanaume kunyong'onyea

Jumatano , 13th Jan , 2021

Mjumbe wa nyadhifa, Paul Mashauri, amesema kuwa hakuna kitu kinachomnyima raha mwanaume kama kukosa pesa, kwani hata ikitokea karudi nyumbani na kuambiwa hakuna kitu fulani huwa ananyong'onyea kabisa.

Mjumbe wa nyadhifa, Paul Mashauri

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 13, 2021, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfsast cha East Africa Radio, ambapo pia ameshauri kwa watu wanaoingia kwenye mahusiano ni vyema kila mmoja wao akamuuliza mwenzake kuhusu matumizi yake ya fedha.

"Ukitaka mwanaume anyong'onyee 'wallet' iwe haina hela, na ndiyo maana mwanaume hata kama 'wallet' haina hela anaibeba tu, uzuri wa akina mama wakishajua baba hana hela wanakuwa creative, atapika hata makande", amesema Paul Mashauri.

Aidha ameongeza kuwa, "Unapoingia kwenye mahusiano muulize mwenzako anaamini nini katika fedha, mwingine amezoea kubana sana mwingine amezoea ku-spend, kama hamjaulizana utakuja kushangaa mwenzako amepata mshahara wote amenunulia viatu".