Alhamisi , 24th Nov , 2022

Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego, amesema yeye pamoja na viongozi wenzake watahakikisha wanakusanya malori yote ya Iringa kwa ajili ya kusambaza mbolea ya ruzuku kwa wakulima ili wasiwe chanzo cha kukwamisha juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 24, 2022, mara baada ya kupokea maandamano ya wakulima wa mkoa huo wakimpongeza Rais Samia kufuatia mbolea ya ruzuku aliyoitoa kwa wakulima ili kuwapa nafuu na kuwaletea tija kwenye kilimo chao.

"Niwapongeze sana viongozi na wakulima wa mkoa wa Iringa, sio kila siku tukikutana ni magomvi tu lakini wakati mwingine binadamu akifanya mazuri ni kumshukuru, ametuletea ruzuku ya mbole ili tuzalishe, mpaka sasa tumesajili asilimia 93 ya wakulima, tumekubaliana kwamba tutakusanya malori yote ya Iringa kuelekeza vijijini kupeleka mbolea," amesema RC Dendego