Jumatatu , 1st Aug , 2016

Ujenzi wa barabara ya Soko Kuu la Majengo Mkoani Dodoma uko mbioni kuanza Kujengwa baada ya kukaa muda mrefu bila matengenezo hali iliyowafanya wafabiashara kushindwa kufanya biashara zao kwa ufanisi.

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Seleman Jaffo.

Ahadi hiyo ujenzi wa barabara hiyo umekuja mara baada ya Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Seleman Jaffo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza sokoni hapo.

Mhe. Jaffo amesema kuwa wakati huu wa serikali ikihamia Mkoani humo haina budi miundombinu yote kuirekebisha kwa kiwango kinachotakiwa ili kurahishaa ukuaji wa uchumi kutokana na watu wanaotarajia kuwasili mkoani humo.

Waziri Jaffo amehoji kwanini barabara hiyo imechukua muda mrefu kufanyiwa matengenezo wakati kuna barabara nyingine ambazo zipo nje ya mji zimefanyiwa ukarabati wa mara kwa mara.

Sauti ya Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Seleman Jaffo.