Jumatano , 21st Oct , 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amezindua uwanja wa ndege katika kambi ya kijeshi ya anga iliyoko Ngerengere mkoani Morogoro huku akisema anajivunia kutoka madarakani akiwa ameiacha nchi katika hali nzuri ya kiusalama.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mirsho Kikwete akiwa na Mkuu wa Majeshi Davis Mwamunyange

Rais Kikwete akizungumza katika uzinduzi huo amesema katika kipindi cha uongozi wake amefanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuliacha jeshi likiwa katika hali nzuri ambapo ameeleza hakuna nchi inayo weza kuwa na maendeleo kama haina Jeshi imara.

Aidha Rais Kikwete amelishukuru jeshi la serikali ya China walio husika kujenga uwanja huo wenye urefu wa mita 3000 ambapo amesema serikali ya China imekuwa rafiki wa Tanzania kwa muda mrefu na serikali ijayo hainabudi kuendeleza mahusiano yaliopo kwa nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi Davis Mwamunyange amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuliimarisha jeshi la Tanzania ingawa zipo changamoto ndogodogo laki anaamini serikali itazifanyia kazi ili kuweza kuwa na jeshi imara.

Naye waziri wa ulinzi Dkt. Husein Mwinyi amesema uwanja huo utaliwezesha jeshi kuweza kufanya mazoezi yake na kuwasaidia wananchi wanaotumia usafiri wa ndege na kuishukuru serikali ya China kwa moyo wao wa kuisaidia Tanzania kwa vitu.