Alhamisi , 6th Oct , 2022

Mwanamke mmoja ambaye hajajulikana, anadaiwa kutoa mimba inayokadiriwa kuwa na miezi mitano hadi sita na kisha kukitupa kiumbe alichokuwa nacho tumboni katika dampo la Wilika, Kata ya Gongoni Manispaa ya Tabora, mkoani Tabora, usiku wa kuamkia leo.

Jalala la Wilika mkoani Tabora

Mmoja wa mashuda ambaye amekuwa na kawaida ya kuendesha shughuli zake za kuokota  chupa za plastiki kila siku mapema asubuhi, amesema baada ya kufika eneo hilo alitatanishwa na aina ya mfuko mpya ambao ulionekana ukiwa umefungwa kifurushi.

Kufuatia tukio hilo Jeshi la Zimamoto mkoani humo, likawaasa wanawake kutokuwa na mioyo migumu inayopelekea hatua za wao kutupa watoto jalalani