Ijumaa , 5th Sep , 2014

Rais wa Tanzania DK. Jakaya Kikwete amesema kuwa atawakusanya viongozi wa mikoa yote yenye migogoro baina ya wakulima na wafugaji ilikuangalia jinsi ya kutatua matatizo yao na kuhakikisha wakulima na wafugaji wanaishi kwa amani.

Rais wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

Akizungumza na wazee, katika majumuisho ya ziara yake mkoani Dodoma Rais Kikwete, amesema kuwa viongozi wa mikoa ya Morogoro Manyara, tanga na Dodoma watakusanywa katika mkutano na kujadili jinsi ya kumaliza migogoro yao.

Mbali na suala la mgogoro huo pia Dk Kikwete amenema kuwa anatarajia kukutana na timu aliyo iunda mkoani Dodoma hivi karibudi ya kuchunguza mgogoro baina ya mamlaka ya ustawishaji makao makuu CDA ili kutatua migogoro iliyopo mkoani humo.

Katika hatua nyingine, vikundi 140 vya wakulima nchini Tanzania kutoka katika mikoa vinatarajia kufaidika kwa kuuza kwa wakala wa chakula kiasi cha tani laki mbili za nafaka.

Hayo yamesemwa na Waziri wa kilimo na chakula Christopher Chiza ambapo amesema ununuzi kupitia vikundi unalenga kufikisha kwa wakulima bei nzuri iliyotolewa na serikali pamoja na kuhamasisha ushirika nchini.

Aidha Chiza amesema changamoto iliyopo kwa sasa ni kwa mazao yanayoletwa na wakulima katika vituo vya uwakala ni kuwa na ubora hafifu, wafanyabishara kununua mahindi kwa wakulima kwa bei ndogo na kuuza kwa wakala kwa bei ya shilingi 500.