Alhamisi , 22nd Sep , 2022

Zikiwa zimebaki siku mbili  kufikia siku 100 tangu kuanza kwa zoezi la wakazi wa Ngorongoro kuhamia Kijiji cha Msomera kwa hiari yao wenyewe kutoka ngorongoro, kundi la kumi leo limeondoka kuelekea Msomera likiwa na kaya 29 na watu 139 na zaidi ya mifugo 700

Kundi hilo linafanya  Jumla ya Kaya 266 zenye watu 1,366 na Mifugo 8,177 kuwa tayari zimeshahamia Msomera .
Kwa mujibu wa Takwimu za Ngorongoro kuhusiana na zoaezi hilo, hadi sasa Kaya zilizozitokeza kujiandikisha na ajili ya kuhama kwa hiari ni 1,372 zenye Jumla ya Watu 7,272 na Mifugo zaidi ya 34,000,ambapo wakazi wanao elekea Msomera leo hii wameonesha tumaini jipya 

Akitoa taarifa ya Maendeleo ya zoezi hilo Naibu Kamishna wa uhifadhi Hifadhi ya ngorongoro Dr Christopher Timbuka amesema hamasa na idadi ya wanaojiandikisha kwa hiari imezidi kupanda siku hadi siku 
Aidha hadi sasa Kaya zilizozitokeza kujiandikisha na ajili ya kuhama kwa hiari ni 1,372 zenye Jumla ya Watu 7,272 na Mifugo zaidi ya 34,000