Jumanne , 22nd Sep , 2015

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia (UKAWA), Mhe. Edward Lowassa amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais ataunda tume kwa ajili ya kuchunguza upya mikataba ya gesi na mafuta.

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia (UKAWA), Mhe. Edward Lowassa.

Akizungumza mkoani leo Mtwara katika mkutano wa hadhara wa kunadi sera za chama hicho katika viwanja vya Mashujaa, uliohudhuliwa na maelfu ya wakazi wa mkoani humo, amesema anafahamu kiu ya wananchi wa Mtwara na namna walivyokerwa juu ya kunufaika na rasilimali hizo.

Kwa upande wake, waziri mkuu mstahafu wa serikali ya awamu ya tatu, Mhe. Fedrick Sumaye, amemtaka mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. John Magufuli, kuhamia UKAWA na kuungana na Lowassa, kwasababu anaonyesha kunogewa na sera na misemo ya CHADEMA.

Amewasisitiza wananchi kutokuwa waoga katika kufanya mabadiliko kwa kuhofia kutokea kwa vurugu, akitolea mfano nchini Libya ambako kulitokea vurugu kwa ajili ya kuipinga serikali ya Muammar Ghadaf, na kusema vurugu hizo zilitokana na serikali hiyo kung’ang’ania madaraka kama ilivyo kwa CCM.