Ijumaa , 6th Nov , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Adelardus Lubango Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Taarifa ya serikali imeeleza kuwa uteuzi wa Kilangi umeanza Novemba 5, 2020.

Aidha Prof. Kilangi ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya uteuzi wa kipindi cha kwanza kumalizika Novemba 5, 2020.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Lubango Kilangi

Jana Novemba 5, Rais Dkt. John Magufuli aliapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya pili ambayo imeanza 2020 na itamalizika 2025.