Jumatatu , 15th Aug , 2022

Mwanamke aitwaye Faustina Kimamba, mkazi wa Kijiji Cha Mapili wilayani Mlele mkoani Katavi ambaye ni mjane amefukuzwa na watoto wake kwenye nyumba na mashamba waliyotafuta na mumewe aliyefariki 2010, baada ya kuanzisha mahusiano na mtu mwingine.

Faustina Kimamba, Mama aliyefukuzwa na watoto wake

Akisimulia kisa kizima cha tukio hilo, mjane huyo amesema alishawishika kuingia kweye mahusiano kutokana na hali ya kiuchumi, watoto wadogo na mwanume huyo alikuwa akimsadia huduma mbalimbali.

Bi Faustina amesema mtoto wake wa pili kumzaa ndiye aliyemfukuza huku akimtupia maneno makali kwa kumuita Malaya.

Mjane huyo ameelezea vitisho na maonyo makali aliyoyapata toka kwa ndugu wa mme yaliyompelekea kupata hofu na kuacha kufuatilia mali hizo huku akiishia kuendelea kutaabika kimaisha.

Baada ya EATV kukinasa kisa hicho, ilimtafta Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo na kumuelezea kisa kizima bila kupepesa macho ambapo amekea vitendo hivyo na kumtaka mhanga kufika ofisini kwake mara moja ili apewe msaada wa kisheria.