Alhamisi , 2nd Dec , 2021

Watoto wawili wa familia moja wakazi wa kijiji cha Mwabagaru Kata ya Buseresere, wilayani Chato mkoani Geita, wamefariki dunia na watatu kunusurika kifo baada ya kunyeshwa sumu ya kuulia wadudu na mama yao mzazi ambaye na yeye alikunywa sumu hiyo kisa ugumu wa maisha.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe

Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe, ameitaja aina ya sumu waliyonyweshwa watoto hao kuwa ni ya kuulia wadudu aina ya Incecron Profenos 720g/L.

Kamanda Mwaibambe ameongeza kwamba watoto watatu na mama yao bado wanapatiwa matibabu kwenye kituo cha Afya Bwanga

Watoto waliopoteza maisha ni Jane Mgema (12) na Janeth Mkama (2).