Alhamisi , 29th Mei , 2014

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF) Eliud Sanga amekanusha madai kuwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe amekopa kiasi cha Sh. Bill. 1 kwenye mfuko huo.

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za mikoa na serikali za Mitaa mhe. Hawa Ghasia. Waziri Ghasia alitoa madai kuwa mfuko wa pensheni kwa wafanyakazi wa serikali za mitaa (LAPF) umemkopesha kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe, kiasi cha Sh. Bilioni moja.

Mdai hayo yaliyotolewa na Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za mikoa na serikali za Mitaa Hawa Ghasia, yameonekana kutokuwa na ukweli wowote.

Pia LAPF imekana kuwasaidia fedha au vifaa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Iringa Mjini Peter Msigwa kama ilivyosemwa bungeni.

Aidha Mkurugenzi Mkuu huyo aliongeza kuwa mfuko huo hauna utaratibu wa kumkopesha mtu mmoja mmoja, hivyo hakuna mikopo ya aina hiyo.