Ijumaa , 21st Jan , 2022

Mchungaji mmoja aliyetambulika kama Curtis Keith Bankston (55) na mkewe Sophia Simm Bankston wamekamatwa kwa madai ya kuwafungia ndani  walemavu nane wa akili ndani ya nyumba yao huko Georgia  nchini Marekani.

Mchungaji Curtis Keith Bankston na mkewe Sophia Simm Bankston

Taarifa zinaeleza kuwa bwana Bankston alidhibiti fedha za walemavu hao, huku akitumia nyumba hiyo kuwaficha walemavu kwa kisingizo cha nyumba yao ni kanisa na yeye ni mchungaji.

Bankston na mkewe walikuwa wakiendesha kituo cha kuwatunza walemvu bila kibali maalumu.