Jumatano , 3rd Sep , 2014

Biashara katika jiji la Dar es salaam zimeanza kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya mgomo wa kupinga matumuzi ya mashine za kutolea risiti za kiletroniki EFD.

Baadhi ya maduka jijini Dar es Salaam yakiwa yamefungwa kutokana na mgomo wa wafanyabiashara wanaopinga mashine za kutolea risiti za kielektroniki maarufu kama mashine za EFD.

Katika kikao walichofanya wafanyabiashara hao na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Said Mecky Sadick kiliazimia kufungulia maduka hayo na kuitaka mamlaka ya mapato Tanzania TRA kukaa na wafanyabiashra ili kumaliza mgogoro huo.

Hata baadhi ya maduka bado ynatoa risiti zisizokua za kieletroniki unaendelea huku TRA ikiendelea kusisitiza Wananchi kutopokea risiti hizo kwa kuwa kufanya hivyo ni ukwepaji wa kodi.

Katika hatua nyingine, wajasilia mali wanawake Zaidi ya 600 jijini Mwanza watapewa elimu ya ujasilia mali katika nyanja za usimamizi wa fedha na uwekaji akiba na mafunzo ya afya bora na uchumi imara.

Mkurugenzi mkuu was AMCL,Naima Malima amesemav katika nyanja ya ujasilia mali imelenga kutoa elimu kwa akina mama hao kuhusu vigezo vya kuzingatia katika kujifanyia tathmini na rasilimali zinazopatika katika eneo husika la bioashara.

Amesema AMCL,kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo Jinsia na Watoto, na Taasisi ya WAMA watawafikia wanawake wa vikundi vyote vya kijamii kama,Saccos,AMCOS,VICOBA na makundi mengine ya ujasilia mali kampeni ambayo ambayo itawaongezea wateja katika biadhaa zao