Taswira ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi.
Takwimu za serikali ya nchi hiyo zinaonesha kuwa kumekuwa na wageni 324,276 kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) na Uwanja wa Kimataifa wa Mombasa (MIA) baina ya Januari na Mei mwaka huu.
Takwimu za Ofisi ya Takwimu Kenya katika ripoti zake za vyanzo vinavyoongoza katika kukuza uchumi, zinaonesha katika kipindi kama hicho mwaka 2015, Kenya ilipokea wageni 284,313 kupitia viwanja vya ndege.







