"Mimi nimhujumu Mbowe kwa kipi"- DC Sabaya

Jumatatu , 19th Oct , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, amesema kuwa yeye hajawahi kumhujumu mgombea ubunge wa jimbo hilo, Freeman Mbowe, kwa namna yoyote ile bali Mbowe amejihujumu mwenyewe kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa wananchi.

Kushoto ni mgombea ubunge wa jimbo la Hai Freeman Mbowe, na kulia ni mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya.

Sabaya ametoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kuongeza kuwa hatohangaika naye kwa namna yoyote ile, bali yeye anaelekeza nguvu zake kwa wananchi wa wilaya ya Hai, kwa ajili ya kuwaletea maendeleo.

"Mimi namhujumu Mbowe kwa kipi, ameshajihujumu mwenyewe kwa kutokufanya wajibu wake, mimi siwezi kumjibu tena nitaendelea kuhangaika na wananchi wanaohitaji maendeleo, siwezi kuhangaika naye anayefanya kampeni asubuhi hadi jioni anatoka kwa Magufuli anakuja kwa Sabaya, yeye atapambana na hali yake mwenyewe amani ya Hai haiguswi na mtu yoyote", amesema DC Sabaya.

Tazama video hapa chini.