Jumatano , 16th Dec , 2015

Mahakama ya wilaya ya Chato mkoani Geita imewakuta na kesi ya kujibu washitakiwa sita ubadhilifu wa pembejeo za kilimo na matumizi mabaya ya madaraka akiwemo aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo,Hadija Nyembo,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kaliua.

aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Geita,Hadija Nyembo,ambaye kwa sasa ni mkuu wa wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora.

Wengine ni aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Hamida Kwikwega,Ofisa kilimo na mifugo wa wilaya Fares Tongora, Wakala wa usambazaji wa pembejeo Mery David pamoja na mtendaji wa kijiji cha Mapinduzi kata ya Buseresere,

Hatua hiyo imekuja baada ya mwendesha mashitaka wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru),Kelvine Murusuri,kufunga ushahidi wa upande wa mashitaka ili kutoa fursa kwa mahakama hiyo kuendelea na taratibu zake.

Akitoa uamuzi huo,hakimu wa mahakama ya wilaya ya chato,Yona Wilson,amesema kutokana na ushihidi uliotolewa tangu awali,mahakama imejiridhisha kuwa washitakiwa wana kesi ya kujibu na kwamba wanapaswa kuanza kutoa utetezi wao kuanzia januari 13 kwaka 2016.

Kesi hiyo ni miongoni mwa kesi zingine 8 za ubadhilifu wa pembejeo za kilimo na matumizi mabaya ya madara ambazo zinawakabili vigogo mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya chato na mawakala pamoja na watendaji wa vijiji ambao wanakabiliwa na makosa mbalimbali.

Katika bajeti ya serikali ya mwaka 2009/2010 serikali kupitia wizara ya kilimo chakula na ushirika ilitoa pembejeo za kilimo zenye thamani ya takribani bilioni 1.5 kwa wilaya ya chato ili kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao na kuwa na tija lakini zaidi ya bilioni 1.3 hazikuwafikia walengwa.