Jumapili , 19th Sep , 2021

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Christina Mndeme amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji kufika Newala siku ya Jumatatu tarehe 20 Septemba, 2021 katika mradi wa maji Makonde ambao haujatoa maji kwa takribani wiki tatu sasa.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Christina Mndeme (katikati)

Amesema hayo baada ya kutembelea kituo cha kupokea maji kutoka kwenye chanzo cha maji Mkunya na kujionea mashine zikiwa zimeharibika.