Jumatatu , 13th Oct , 2014

Moto uliowaka zaidi ya masaa 9 umeteketeza meza zaidi ya 250 na maduka zaidi ya 330 ya wafanyabiashana, huku wananchi wakihangaika kuuzima kwa kutumia mchanga, katika soko kuu la mji mdogo wa Urambo mkoni Tabora usiku wa kuamkia leo.

Sehemu ya Soko la Urambo

Moto uliowaka zaidi ya masaa 9 umeteketeza meza zaidi ya 250 na maduka zaidi ya 330 ya wafanyabiashana, huku wananchi wakihangaika kuuzima kwa kutumia mchanga, katika soko kuu la mji mdogo wa Urambo mkoni Tabora usiku wa kuamkia leo, katika kile, kilichohisiwa kuwa, unaweza kuwa umesababishwa na mamarishe ndani ya soko.

Wakiongea kwa masikitiko baadhi ya wafanyabiashara walioathiriwa na moto huo, katika soko hilo wameiomba serikali kujitahidi kuwatenda akina mama lishe na mafundi wa kushona nguo kuwaondoa katikati ya maduka na meza kwani inawezekana kuwa, waliacha moto ukiwaka, na kusababisha hasara ya mamilioni ambayo haikupatikana mara moja.

Aidha akizungumzia changamoto iliyowakumba wananchi wa kata hiyo kutokana na hasara ya mamilioni, waliyoipata, diwani wa kata hiyo ya Urambo mjini Bw. Amatus Liumba ameomba wananchi kujenga tabia ya uaminifu kwani katika kuokoa mali nyingi zilihamishwa katika njia za panya na kutoweka.

Juhudi za kumpata afisa biashara wa wilaya Bw. Hatibu Abdulrahman ili kujua kiasi cha hasara walioipata wafanya bishara hao zinaendelea kutokana na tathmini zinazoendelea kufanyika.